Beki wa zamani wa
klabu ya Manchester United na timu ya taifa ya Uingereza Gary Neville
amefutwa kazi na klabu ya Valencia ya Uhispania baada ya kuhudumu kama
meneja wao kwa chini ya miezi minne.
Valencia walishinda mechi tatu pekee kati ya 16 walizocheza ligini chini ya Neville, na mechi 10 kati ya 28 kwa jumla katika mashindano yote.
Neville amesema alitaka sana kukaa Valencia lakini matokeo hayakufikia kiwango chake na viwango vinavyohitajika na klabu hiyo.
Ameongeza kwamba anafahamu wazi kwamba “tumo katika biashara ya kuangalia matokeo”.
Ndugu yake mdogo, Phil, amekuwa kwenye benchi ya kiufundi Valencia na ataendelea na kazi yake.
Neville alianza kutakiwa ajiuzulu baada ya klabu hiyo kucharazwa 7-0 na Barcelona mechi ya kwanza ya nusu Copa del Rey mwezi Februari.

Post a Comment