0


Mwanariadha kutoka nchini Kenya aliyeshinda medali ya shaba kwenye riadha na kuruka vihunzi pamoja na maji, Ezekiel Kemboi amepokonywa medali yake kwa kosa la udanganyifu mchezoni kwenye mashindano ya Olimpiki yanayoendelea huko nchini Brazil.

Kemboi (34) alimaliza kwenye nafasi ya tatu ya mashindano hayo ya kukimbia ya mita 3000 kwa kutumia muda wa 8:08.47. Ufaransa ilipinga ushindi huo wa Kemboi kwa kukata rufaa baada ya kubainika kuwa mwanariadha huyo wakati akiendelea na mbio hizo baada ya kuruka kiunzi na maji, alikanyaga nje ya mstari.

Kamati ya mashindano hayo imekubali rufaa hiyo na kuamuru kumpatia medali hiyo ya shaba, Mahiedine Mekhissi kutoka Ufaransa aliyeshika nafasi ya nne baada ya kukimbia kwa muda wa 8:11.52.

Hata hivyo Kemboi ambaye alikuwa bingwa wa mbio hizo kwenye mashindano ya Olimpiki ya 2012 ya nchini Uingereza amedaiwa kutangaza kustaafu kucheza mchezo huo.

Post a Comment

 
Top