Baada ya madai kuwa msanii wa filamu, Steve Nyerere alikuwa na matumaini ya kuteuliwa na Rais Dk. John Pombe Magufuli katika uteuzi wa wakuu wa wilaya (ma-DC) wapya, staa huyo wa filamu amefunguka na kuzungumzia issue hiyo.
Steve Nyerere
Steve Nyerere amesema yeye ni mmoja kati ya watu ambao walikuwa wanasubiria uteuzi wa ma- DC na hajajisikia vibaya kukosa kwa kuwa ana imani bado Magufuli anamwangalia.
“Mtu kama upo smart kwanini usisubirie nafasi kama hizo, mimi ni mtu safi na kazi naiweza,” alisema Steve.
Aliongeza, “Uteuzi nimeusikia, tuombe mungu kama akinifikiria kwa awamu nyingine sio mbaya, tena ningependa Kinondoni, ni sehemu ambayo naona naweza kuifanyia kazi vizuri kwa sababu hata kwenye nafasi za ubunge nilishika nafasi yatatu, kwa hiyo kama ningepata Kinondoni ingekuwa poa zaidi”
Mwigizaji huyo ni mmoka kati ya wasanii ambao walikuwa katika team ya kampeni ya Magufuli katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2016.
Post a Comment