Hatimaye
Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) imetangaza
nauli zitakazo tumika kwa mabasi yaendayo kasi kuwa ni 400, 650 na 800
kwa safari za Mbezi mwisho hadi Kivukoni.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Mkurugenzi Mkuu wa SUMATRA, Giliard Ngewe amesema nauli kutoka Mbezi mwisho hadi Kimara Sh400, na nauli ya Sh650 itatumika maeneo ya Kimara kwenda Kivukoni, Kimara –Kariakoo, Kimara – Morocco, Kariakoo - Kivukoni.
Amesema
nauli ya Sh800 ni Mbezi Mwisho-Kimara –Kivukoni, kivukoni-Kimara- Mbezi
Mwisho, Mbezi Mwisho-Kimara- Kariakoo, Kariakoo-Kimara-Mbezi Mwisho,
Mbezi Mwisho Kimara- Morocco,na Morocco- Kimara-Mbezi Mwisho.
“Chombo
chochote cha usafiri hakitaruhusiwa kutumia barabara za mwendo kasi
kuanzia kesho, watakao kiuka agizo watachukuliwa hatua za kisheria ikiwa
ni pamoja na kufutiwa leseni za biashara zao” amesema.
Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA)
Bw. Giliard Ngewe akiongea na waandishi wa Habari (hawapo pichani)
kuhusu nauli zitakazotumika katika mradi wa mabasi yaendayo haraka
unaotarajiwa kuanza rasmi Mei 10, 2016. Kushoto ni Mkurugenzi wa
Udhibiti Uchumi kutoka SUMATRA Bw. Nahson Sigala.
Mkurugenzi
wa Udhibiti Uchumi wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Majini na Nchi
Kavu (SUMATRA) Bw. Nahson Sigala akiwaeleza waandishi wa habari kuhusu
viwango vipya vya nauli baada ya SUMATRA kufanya tathmini ya viwango vya
nauli iliyopendekezwa awali na Kampuni ya Usafirishaji ya UDA-RT na
kubaini kuwa gharama zilizopendekezwa ni kubwa mno. Kulia ni Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA) Bw.
Giliard Ngewe.
Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA)
Bw. Giliard Ngewe (Kulia) na Kaimu Mtendaji Mkuu DART Bw. Ronald
Lwakatare wakimkabidhi leseni ya usafirishaji Mkurugenzi Mtendaji wa
Kampuni ya Usafirishaji ya UDA-RT Bw. David Mgwassa (Katikati)
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya Usafirishaji ya UDA-RT Bw. David Mgwassa
(Kushoto) akimshukuru Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa
Majini na Nchi Kavu (SUMATRA) Bw. Giliard Ngewe baada ya kupokea leseni
ya usafirishaji kutoka SUMATRA.
Post a Comment