Aliyekuwa winga wa timu ya Ufaransa
David Ginola anaendelea kupata afueni hospilini mjini Monaco baada ya
kufanyiwa upasuaji wa moyo.
Daktari aliyemfanyia upasuaji huo amesema kuwa Ginola alinusurika kifo.
Ujumbe wa Twitter kutoka kwa nyota huyo wa zamani ulisema: Walimwengu hamjambo,sikulala vizuri.Niko salama ,ijapokuwa nataka kupumzika kiasi.
David alicheza katika mechi ya hisani .Lakini ghafla akaanguka na kuzirai huku watu wakidhani ilikuwa mzaha lakini baada ya dakika mbili wakabaini mchezaji huyo yupo hatarani,alisema Gilles Dreyfus,profesa wa upasuaji katika hospitali ya kukabiliana na magonjwa ya moyo huko Monaco
Post a Comment