0


                     Hanafi alikuwa afisa wa habari wa kundi la al-Shabab
Mwanahabari aliyesaidia kundi la al-Shabaab kuua wanahabari wenzake nchini Somalia ameuawa.
Hassan Hanafi ameuawa kwa kupigwa risasi mapema asubuhi baada ya kuhukumiwa kifo na mahakama ya kijeshi nchini humo.

Hassan Hanafi, alipatikana na hatia ya kuwaua Sheikh Noor Mohamed Abkey (mhariri wa shirika la habari la SONNA),

Sa'id Tahlil Warsame (mkurugenzi wa HornAfrik), na Mukhtar

Mohamed Hirabe (mkurugenzi wa Radio Shabelle), na wanahabari wengine kadha.

Alikamatwa nchini Kenya Agosti mwaka 2014 na kupelekwa Somalia mwishoni mwa mwaka jana.
Alihukumiwa kifo na mahakama ya kijeshi ya ngazi ya chini nchini Somalia tarehe 3 Machi.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, maafisa wa jeshi wamesema mwanahabari huyo alikiri mauaji ya wanahabari watano.

Mahakama ya juu ya kijeshi iliidhinisha hukumu hiyo tarehe 26 Machi kwa mujibu wa kituo cha redio cha Radio Mogadishu.

Hukumu dhidi yake imetekelezwa siku mbili baada ya mahakama ya kijeshi kuwaua wanahabari wawili waliopatikana na hatia ya kumuua mwanahabari wa kike Hindiyo Hajji Muhammad Khayre.
Wawili hao, walitambuliwa kama Abdirisaq Muhammad Barrow Addow na Hasan Nur Ali Farah, walipatikana na hatia ya kutegwa bomu kwenye gari la Khayre tarehe 3 Desemba 2015.

Post a Comment

 
Top